VITA VYA AFRIKA

Zipo nchi mbambali ambazo kuna machafuko kila mda na kila kukicha; watu wasio na hatia wanauliwa kila mara, watoto wanateseka wakina mama wanabakwa na mengine mengi yanatokea kisa vita!!!!! 


Namuomba mungu nchi zetu za Afrika tufike wakati tuishi kwa amani, haipendezi kuona watoto wasiojua kitu na wasikuwa na hatia kuuliwa, wala mabinti, wanawake, mama zetu kubakwa na kuuliwa. Haipendezi kuona nchi ya Congo, Sudan, Libya n.k watu kukimbia makazi yao; inatia huruma sana.

Pia naiombea nchi yangu ya Tanzania tudumishe amani, tusijigawe kutokana na sababu zozote zinazo tukumba, kumbuka siasa, dini, wala kabila, havina faida sawa na utu wa mtu.


Watanzania tujiepushe na chochezi au nguvu kutoka nje maana siku zote hayupo aliyemtesa babu yako wakati wa ukoloni, atakayekupenda leo. 


Tujiepushe na watu wenye kuchafua na kuvuruga nchi yetu maana hii amani ikija kupotea, hayupo atakaye weza kulima, kufuga, kufanya biashara, wala kufanya kazi yoyote ya kumuingizia kipato; hivyo tutakuwa tumeita matatizo katika jamii yetu.


Hakika kumbukenj, vita haiana faida zaidi kama faida tunazopata tukiwa na amani, licha ya kuwa zipo faida za uwepo wa faida za vita, ila bora tuzidi kuwa na vurugu ndondogo za ndani ila sio vurugu za kutumia zana za kivita na kuuana.


"AMANI KUITOA KATIKA JAMII YAKO NI MUDA MFUPI SANA, ILA IKISHATOWEKA NI MIAKA MINGI SANA KUIRUDISHA".



By Ediga.


Hayapo maendeleo bila amani. 

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii