TAARIFA KWA VIJANA WA TANZANIA
Taarifa kutoka Pro-youth reformer 1
Kila Kijana wa Kitanzania anapaswa kuwa na ajira, ila tu asiwe mzembe kufikiria, na kuwajibika kutokana na alivyofikiri. (Fikiri sasa uajiliwe au ujiajiri mwenyewe!?)
UNAWEZA!! USIJIDHARAU.
Tanzania mpya ni ya vijana wenye ajira zenye tija, lakini vijana wengi Wanashindwa kujua yafuatayo:-
1. Vijana wanapaswa kuwa na ujuzi ndipo watafute ajira. (Kama unataka maendeleo yako uyafikie basi anza kujielimisha na upate ujuzi). Hayupo atakaye kuajiri ikiwa huna ujuzi.
Hakuna mtu ambaye anaweza kuajiliwa bila kujiweka kwenye mazingira ya kuhudumu.
2. Vijana wengi huathiriwa na mwangwi wa mila na tamaduni zao huku wakisahau kubadilisha kwa nyakati. Na pia utofauti uliopo Kati ya ajira zilizopo katika mazingira yao.
Aina za ajira ambazo zinaweza kuajili vijana wengi
1: Zisizo rasmi.
2: Zilizo rasmi.
'muda fulani watu hujiingiza katika majukumu yasiyo na tija ili na wao waonekane kuwa wanawajibika huku hakuna tija kwa wayafanyayo'.
"AMKA"""
#ANZA SASA USHINDE
Maoni
Chapisha Maoni