Zipo nchi mbambali ambazo kuna machafuko kila mda na kila kukicha; watu wasio na hatia wanauliwa kila mara, watoto wanateseka wakina mama wanabakwa na mengine mengi yanatokea kisa vita!!!!! Namuomba mungu nchi zetu za Afrika tufike wakati tuishi kwa amani, haipendezi kuona watoto wasiojua kitu na wasikuwa na hatia kuuliwa, wala mabinti, wanawake, mama zetu kubakwa na kuuliwa. Haipendezi kuona nchi ya Congo, Sudan, Libya n.k watu kukimbia makazi yao; inatia huruma sana. Pia naiombea nchi yangu ya Tanzania tudumishe amani, tusijigawe kutokana na sababu zozote zinazo tukumba, kumbuka siasa, dini, wala kabila, havina faida sawa na utu wa mtu. Watanzania tujiepushe na chochezi au nguvu kutoka nje maana siku zote hayupo aliyemtesa babu yako wakati wa ukoloni, atakayekupenda leo. Tujiepushe na watu wenye kuchafua na kuvuruga nchi yetu maana hii amani ikija kupotea, hayupo atakaye weza kulima, kufuga, kufanya biashara, wala kufanya kazi yoyote ya kumuingizia kipato; hivyo tutakuwa...